|
Karibu Habari mpya Undugu wetu Tunahusiana na nani Jimbo la Biedenkopf Jimbo la Kituntu EKHN KKKT Ujerumani na Tanzania Maeneo ya Kazi Ziara Mbalimbali Jumapili ya Undugu Miradi yetu Mambo ya Umoja Tathmini Wasiliana nasi Wahariri Tovuti nyinginezo Tuunge Mkono
![]() |
Tu wamoja: Masuala ya Uekumene
Undugu unatuwezesha kujifunza na kufanya kazi kwa pamoja kwa njia mbalimbali, au kile kiitwacho uekumene. Wengi wetu, Wajerumani kwa Watanzania, tunaoshiriki katika undugu huu, tunafahamu kwamba sisi ni ndugu, tunaoishi katika dunia moja isiyogawanyika. Na kama jimbo, usharika au mtaa, sisi ni sehemu ya kanisa la Kristo lililoko ulimwenguni kote. Kukutana na watu toka mataifa mbalimbali na tamaduni mbalimbali kunakuza ufahamu wa kila mmoja wetu kuhusu dunia, na pia unaimarisha imani na maisha yetu mazima. Hivyo, iwe Ujerumani au Tanzania, tunaitwa kujifunza kufikiri kama watu wa dunia moja, lakini wanaopaswa kutenda kazi kutegemeana na mazingira tunamoishi.
|
||||