|
Karibu Habari mpya Undugu wetu Tunahusiana na nani Jimbo la Biedenkopf Jimbo la Kituntu EKHN KKKT Ujerumani na Tanzania Maeneo ya Kazi Ziara Mbalimbali Jumapili ya Undugu Miradi yetu Mambo ya Umoja Tathmini Wasiliana nasi Wahariri Tovuti nyinginezo Tuunge Mkono
![]() |
![]()
Neno „Kituntu“ lina maana nyingi:
1. Kituntu inamaanisha ukanda wa juu. 2. Kituntu ni jina la kijiji, kinachopakana na vijiji vya Katembe na Rwambaizi, nk. 3. Kituntu ni usharika mmojawapo katika dayosisi ya Karagwe. Umbali kutoka Bukoba hadi Kituntu ni karibu kilometa 120, kati ya hizo, ni kilometa 40 tu zenye barabara ya lami. Inachukua karibu masaa 3 kwa gari kufika kijijini Katembe, ambapo kuna makao makuu ya Jimbo. Jimbo la Kituntu lina muundo ufuatao: Kila usharika unaongozwa na Mchungaji. Sharika zimegawanyika katika mitaa, ambayo huongozwa na wainjilisti. Mtaa mmoja una kati ya washarika 50 na 600. Theluthi mbili ya waumini wote ni watoto na vijana. Watu wengi, hasa akina mama, vijana na watoto hushiriki katika ibada kila jumapili. Kwaya mbalimbali huimba kila jumapili kwenye ibada, jambo linalofanya ibada kuwa kivutio zaidi kwa wakristo.
Historia ya Jimbo la Kituntu Mch. Lanky, Mmisionari toka Ujerumani, ndiye Mlutheri kwa kwanza kuhubiri Kituntu. Hii ilikuwa mwaka 1937. Mwaka 1938 wakristo 4 wa kwanza walibatizwa. Wakristo hao walikutana kwenye nyumba ya mkuu wa eneo hilo, Omwani-Kalangi, pale Igurwa kufanya ibada. Idadi ya Wakristo iliongezeka na hii ikapelekea kufungua mitaa ya Runyaga, Katembe, Kishoju, Kinyinya na Maguge. Mwaka 1962 mitaa hii 6 iliunda Usharika wa Kituntu, chini ya uongozi wa Mch. Finn Allan Peterson toka Denmark. Mitaa mingine ilifunguliwa kadri washarika walivyoongezeka. Mwaka 1974 usharika mwingine ulianzishwa, yaani Usharika wa Kihanga. Usharika wa Runyaga ulianzishwa mwaka 1984, miaka mitano baada ya kuzinduliwa kwa dayosisi ya Karagwe. Jimbo la Kituntu pia lilizinduliwa mwaka huo huo. Usharika wa Rugela umeanzishwa baadaye, yaani mwaka 2002. Kabla ya hapo, ulikuwa sehemu ya usharika wa Kihanga. ![]() ![]() |
||||||||||||