|
Karibu Habari mpya Undugu wetu Tunahusiana na nani Jimbo la Biedenkopf Jimbo la Kituntu EKHN KKKT Ujerumani na Tanzania Maeneo ya Kazi Ziara Mbalimbali Jumapili ya Undugu Miradi yetu Mambo ya Umoja Tathmini Wasiliana nasi Wahariri Tovuti nyinginezo Tuunge Mkono
![]() |
KKKT
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
KKKT linao Washiriki takribani milioni nne. Makao makuu yake yapo Mjini Arusha. Linazo dayosisi zipatazo 20 ikiwemo Dayosisi ya Karagwe. Uongozi Mkuu wa kanisa, ambaye huchaguliwa miongoni mwa Askofu, ataliongoza kanisa kwa kipindi cha miaka minne. Kwa sasa ni Askofu Alex Gehaz Malasusa, aliyechaguliwa mwezi Julai 2007. Vikao vya Kanisa Mkutano mkuu ndicho kikao cha juu chenye maamuzi ya KKKT na hukutana kila baada ya miaka minne. Chini yake kuna Halmashauri Kuu ya Kanisa (H/K), ambayo hukutana mara tatu kwa Mwaka. H/K inawajumuisha: Maaskofu wote walioko kazini Makatibu wakuu au wawakilishi wa Wakristo wasio wachungaji. Wakuu au Wakurugenzi wa vituo vya Kanisa. Dayosisi ya Karagwe Dayosisi ya Karagwe (DKAR) ilianzishwa mwaka 1979 kutoka Dayosisi ya Kaskazini Magharibi. Dayosisi hii ipo katika sehemu duni kiuchumi. Miundombinu kama vile barabara, umeme, maji, magazeti na huduma za afya ni duni. Hali hii inaathiri dayosisi na majimbo yake kwa sababu ya mapato hafifu. Ni ukweli kuwa washarika ni fukara katika dayosisi yote na wana hali ngumu ya maisha. Kuanzia Mwaka 2003 dayosisi inaongozwa na Askofu Dr. Benson Bagonza. DKAR inao washarika 85,873 waliogawanyika katika majimbo 7. Inao wachungaji 42 (saba kati yao wako masomoni) na Wachungaji 10 wastaafu. Pia ina masista 12, Madiakonia wa kike 5 na diakoni wa kiume mmoja, na Wainjilisti 205. Kama lilivyo Jimbo la Biedenkopf, Majimbo ya Arsberg, Selters and Nassau , Guetersloh, Leverkusen , Luebeck and Gladenbach (pia ya Ujerumani) yana undugu na majimbo mengine katika DKAR. Kwa mfano, Jimbo la Gladenbach lina undugu na Shule ya Diakonia Nkwenda na Misioni ya Ngara. ![]() ![]() |
||