EKHN



Kanisa la Kiinjili la Hessen na Nassau (EKHN) liko katikati ya
nchi ya Ujerumani. Kanisa hili limeenea pia katika maeneo ya Kusini ya
Mikoa ya Hesse na Rheinland-Pfalz inayounganisha pia eneo la Rhein-Main
na jiji kubwa la Frankfurt. Maeneo ya vijijini ya Vogelsberg, Taunus,
Odenwald na Rothaargebirge/North-Hesse ni sehemu pia ya kanisa hili.


Wakazi takriban milioni 5 wanaishi katika miji na vijiji vinavyohudumiwa na kanisa hili. Milioni 2
kati yao ni washiriki wa kanisa la EKHN. Aidha watu milioni 1.5 ni wa madhehebu mengine.

Kwa mujibu wa Rais wa EKHN, Dr. Peter Steinacker, mambo yafuatayo ni muhimu kwa kanisa:

Imani moja na kushiriki katika kutoa huduma za jamii

Uhai wa kiroho na ushirikishwaji, kwa njia ya mali na vipawa mbalimbali kote nchini.

Kujihusisha na mambo ya kiuchumi na miradi endelevu

Kutunza uumbaji wa Mungu, yaani Uwakili.

Kupungua kwa waumini wa kanisa la EKHN na makanisa mengine nchini Ujerumani ni changamoto
kwa kanisa kuendelea kutoa ushuhuda wake juu ya tumaini katika Yesu Kristo (1. Petro 3:15b).

Tangu yalipofanyika mabadiliko katika muundo wa kanisa miaka ya tisini,
kanisa lina ngazi kuu tatu ka ifuatavyo:

Sharika na mitaa yake

Majimbo: Kwa mabadiliko hayo, majimbo yamepewa uwezo zaidi kushughulikia masuala ya ajira na
maslahi ya wachungaji, wadiakoni, na watumishi wengine katika nyanja za mahusiano (uekumene)
na mambo ya jamii.

Kanisa zima (EKHN): Litakuwa na Sinode, yenye vikao vyake mara mbili kwa mwaka, Halmashauri
Kuu, Rais wa Kanisa pamoja na Maaskofu 6 wa Mikoa.

EKHN na makanisa mengine 23 nchini Ujerumani yanaunda Kanisa la Kiinjili la Ujerumani,
liitwalo EKD. EKD ni mwanachama wa Jumuiya ya Makanisa Duniani.

EKHN ina mahusiano na makanisa na sharika ngambo ya nchi kama vile: Poland, Jamhuri ya
Czech, Italia, Afrika ya Kusini, Tanzania, Ghana, India, Indonesia na Korea ya
Kusini Endelea

Karte

endelea_mbele
  © by Design4Web 2008