|
Karibu Habari mpya Undugu wetu Tunahusiana na nani Jimbo la Biedenkopf Jimbo la Kituntu EKHN KKKT Ujerumani na Tanzania Maeneo ya Kazi Ziara Mbalimbali Jumapili ya Undugu Miradi yetu Mambo ya Umoja Tathmini Wasiliana nasi Wahariri Tovuti nyinginezo Tuunge Mkono
![]() |
![]()
Jimbo la Kiinjili la Kilutheri Biedenkopf lina zaidi ya Wakristo 27.000 wanaoishi kwenye sharika 28. Jimbo hili linaanzia Bromkirchen kwenye bonde la mto „Obere Edertal“ mpaka Breidenbach kwenye bonde la mto Lahntal. Hivyo linaweza kuitwa „ kichwa “ cha kanisa la Kiinjili Hessen na Nassau. Hessen ni mojawapo ya Mikoa (federal states) kumi na sita ya Ujerumani. Kanisa liko katika maeneo ya vijijini, hivyo utakuta jengo la kanisa katikati ya kila kijiji. Makanisa mengi yamejegwa kwa mbao kwa mtindo ujulikanao kama „ Mittelhessen coffee grinders style “. Eneo hili lina historia ndefu ya mapokeo ya Kilutheri. Hata hivyo Uamsho uliingia mkoani hapa katika karne ya 19 na kuleta mabadiliko makubwa katika uchaji wa Wakristo.
Ukilinganisha na maeneo mengine, kuna mahudhurio mazuri katika ibada ya kila jumapili. Makanisa mengi yanajaa. Takwimu zinaonyesha kuwa kuna wastani wa waumini 2.500 wanaohudhuria ibada kila jumapili. Zaidi ya hayo, sharika nyingi zina watendakazi wengi wa kujitolea. Uendeshaji wa kanisa katika eneo hili ni wa Kidemokrasia. Kuna ushirikiano mkubwa kati ya sharika na Jimbo. Halmashauri ya kila usharika huchagua wawakilishi wake kwenye sinode na vikao vinginevyo vya jimbo.
![]()
|