Karibuni sana!
 
     
kwenye tovuti ya Undugu kati ya Jimbo la Biedenkopf - Ujerumani na Jimbo la Kituntu-Tanzania  
     
Jimbo la Kiinjili la Kilutheri Biedenkopf  
Jimbo la Kiinjili la Kilutheri Biedenkopf lina zaidi ya waumini 27.000 ambao wamegawanyika katika mitaa 28. Jimbo hili liko katika eneo la Nordhessen na ni sehemu ya kanisa la Kiinjili la Hessen na Nassau (EKHN).

Mchungaji wa Jimbo ni Mch. Gerhard Failing na Mwenyekiti wa Sinode Jimboni ni Ndugu Frank Schmitt.
   
Jimbo la Kiinjili la Kilutheri Kituntu
Jimbo la Kituntu liko katika ya Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Ni jimbo lenye waumini takribani 8.000 waliogawanyika katika sharika nne zenye jumla ya mitaa 24. Jimbo hili linapatikana Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, yaani katika mkoa wa Kagera, ulioko mpakani mwa Rwanda na Uganda.

Mchungaji wa Jimbo anaitwa Mch. Anatory Kagaruki.
  © by Design4Web 2008